
ILiKUWa siku mbaya kwa timu ya Panama girls ya iringa ilipojikuta wavu wake ukitikiswa mara 10 na wachezaji wa Simba Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa juzi alhamisi katika dimba la Samora, iringa.Mrundi, Asha Djafar alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza katika dakika ya nne ya mchezo, ambapo alifunga mengine mawili dakika ya 11 na 24 na kukamilisha hat-trick yake ya pili msimu huu.
Mabao mengine yaliwekwa kimiani na Neema Paul aliyefunga mawili, Opah Clement, Mwanahamisi Omary Gaucho, Violeth Thadeo, Joelle Bukuru na Stellah Kingwe wote walifunga bao mojamoja.
Hiki ni kipigo cha pili kikubwa kwa Panama Girls ndani ya wiki moja, kwani kabla ya mchezo huo, Juni 29 walifungwa mabao 11-1 na Mlandizi Queens kwenye dimba hilo hilo. Mechi nyingine ya juzi, Ruvuma Queens walibanwa mbavu na Mlandizi na kutoka nao sare ya bao 1-1- katika Uwanja wa Majimaji, Songea.
Kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi, alisema kuwa: “Mako-cha wote wa Simba ambao tume-bakia tuna deni kubwa la kuzipa ubingwa timu zetu, mimi kocha wa timu ya wanawake na makocha wa timu za vijana, tunadaiwa makombe kwa sababu wakubwa zetu wame-shamaliza kazi, nime-waambia vijana wangu kila mch-ezo kwetu ni fainali.

”Kwa matokeo hayo, Simba Queens wamepanda hadi kileleni wakiwa na pointi 35, baada ya michezo 13. Nafasi ya pili JKT Queens na pointi 29 michezo 13, Ruvuma Queens nafasi ya tatu pointi 28.