Maonyesho ya biashara ya kimataifa ya SABASABA bado yanaendelea katika viwanja vya Sabasaba, Dar es salaam, ambapo yalizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 3, July 2020.
Katika maonyesho hayo kampuni inayozalisha bidhaa bora kabisa ya Azania Group nao wamepiga kambi kwenye maonyesho hayo. Ukifika kwenye banda la Azania utakutana na bidhaa zote bomba kama vile mafuta ya kupikia, sabuni, unga wa ngano na sembe, pamoja na bidhaa nyingine ambazo zina ubora wa kimataifa.

Ukifika SABASABA Azania wapo mkono wa kushoto karibu na geti la kuingilia, watembelee ukajionee na kujipatia bidhaa Bora kabisa kwa mahitaji yako ya kila siku.
Tazama Yanayoendelea Kwenye Banda la Sabasaba