×

Rose Ndauka Atoa Siri Ya Maisha Yake

MSANII wa Bongo Muvi, Rose Ndauka ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, amesema kuwa kuna vitu aliamua kuviacha kama; utoto, maisha feki na mambo yake yakaanza kumnyookea.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Rose alisema kuwa, hiyo ndiyo siri iliyomfanya afanikiwe hadi kupata heshima ya ndoa na jamii kwa ujumla.

“Unajua huko nyuma unaweza usijue kama kuna maisha yanatakiwa yasonge mbele ili maisha yako yabadilike, lakini kama hauko tayari kubadilika kiakili, basi hauwezi kusonga mbele hata kidogo.

 

Niliamua kuacha utoto na kukubali kuwa mama Naveen basi, kila kitu naona kimenyooka na sasa ni mke wa mtu,” alisema Rose Ndauka ambaye hana muda mrefu kwenye maisha ya ndoa.

Leave a Comment