×

Samatta Uso Kwa Uso Na Van Dijk

STRAIKA Mtanzania anayecheza Aston Villa, Mbwana Samatta, leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakacho pambana na mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool ambao ukuta wao unaongozwa na Virgil van Dijk.

Katikamchezo huo wa ligi unaotarajiwa kuanza saa 12:30 jioni, utachezwa kwenye Uwanja wa Anfield, sehemu ambayo Samatta aliwahi kwenda hapo na kufunga bao moja wakati akiitumikia KRC Genk kabla ya Januari, mwaka huu kutua Aston Villa.

Wengi watasubiri kuonaSamatta na Van Dijk vita yao itakuwaje kwani awali walipokutana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool ikiifunga KRC Genk mabao 2-1, Novemba 5, 2019, Samatta alifunga bao la kichwa katika ukuta uliokuwa ukiongozwa na beki huyo.

Leo Aston Villawatakuwa na kibarua kizito mbele ya Liverpool kwani timu hiyo inapambana kujinasua na janga la kushuka daraja ikiwa nafasi ya tatu kutoka mkiani na pointi zake 27 walizopata kupitia michezo 32.

Liverpool inatarajiwakuingia kwa hasira zote kutokana na kudhalilika katika mchezo uliopita ilipocheza ugenini dhidi ya Manchester City baada ya kupigwa mabao 4-0

Leave a Comment