×

Rwanda Kufungua Mipaka Agosti 1

Rwanda wamefikia azimio la kufungua viwanja vya ndege mwanzoni mwa Agosti huku wakisistiza upimwaji wa virusi vya Corona kama moja ya kigezo cha kuingia nchini humo.

Rwanda ilisitisha huduma hiyo ya usafiri wa ndege zinazoingia au kutoka tangu mwezi Machi huku ikiruhusu ndege za mizigo tu kutua kwenye ardhi hiyo.

Hata hivyo wasafari wote watakaofika nchini humo itawalazimu kuonyesha majibu ya vipimo vyao vikionyesha kuwa hawana maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwenye maabara iliyoidhinishwa.

“Kwa abiria wanaoingia Rwanda, watafanyiwa tena vipimo pindi tu watakapowasili, huku matokeo yakitolewa ndani ya saa 24 na katika kipindi hicho watakuwa kwenye hoteli zilizotengwa kwa gharama zao wenyewe,” serikali imesema.

Leave a Comment