
Kampuni ya mawasiliano ya tigo imewataka wananchi kutumia nafasi ya uwepo wa maonesho ya kibiashara ya 44 ya Dare salaamu sabasaba kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vifaa vya mawasiliano vyenye ubora kufuatia maonesho hayo kuhusisha kampuni za mawasilianobza simu ambazoZinaleta vifaa vyenye ubora

Akizungumza leo jijini Dare salaamu Meneja wa bidhaa za intaneti kutoka tigo mkumba myonga amesema katika maonesho hayo wameingia makubaliano na baadhi ya kampuni za uuzaji vifaa vya simu ambazo zina sifa na ubora kwa matumizi ya watanzania.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano kutoka kampuni ya Tecno Erick mkomoye ameeleza kuwa hivi Sasa Watanzania wanahitaji teknolojia za Hali ya juu kwenye simu zao wanazotumia ili kuendeleza uchumi wa Kati uliofikiwa na kuifanya endelevu na kwa kutambua hilo wameamua kuja na simu aina ya Tecno spark 5 yenye thamani sawa na mahitaji ya watumishi.
matukio katika picha;
