
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akifuatana na mkewe, Mary Majaliwa, amechukua fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, leo Jumatano, Julai 15, 2020.

Amekabidhiwa fomu hizo na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Ruangwa, Barnabas Essau, katika Ofisi CCM ya wilaya hiyo

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)