
KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameweka wazi kuwa kesho Julai 16, 2020, watamtambulisha rasmi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe, kuwa mwanachama rasmi wa chama hicho.
Zitto ameweka wazi hayo kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa twitter akiwa ameweka picha ya Membe hukuaakiwa ameshikilia kitabu cha ACT-Wazalendo.
Amesema, Membe atatambulishwa kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mlimani City mbele ya wanachama wa chama hicho. Kwa muda mrefu sasa Membe amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye chama cha ACT-Wazalendo baada ya kufukuzwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kukiuka baadhi ya taratibu za chama hicho.
