
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba amefanya ziara ya siku mbili Mkoani Morogoro kukagua Miradi ya maendeleo iliyo chini ya wizara ya kilimo ambapo katika ziara hiyo Mgumba alikagua maendeleo ya uendelezaji wa shamba la miwa la Mkulazi holding Company Limited Kampuni Tanzu ya NSSF.

Utayarishwji wa kitalu ulianza tangu mwezi wa tatu mwaka huu na upandaji wa kitalu cha miwa utaanza mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu 2020.
Kwa sasa limelimwa eneo la hekta 200 na kuanza kuanda kitalu S cha 25 ha na baada ya miezi sita kuhamishiwa kwenye kitalu B cha hekta 200 ha na kuhamishiwa kwenye shamba kuu la mwanzo la hekta 5000ha.
Kiwanda cha mkulazi holding comoany Limired kitakachokuwa kikubwa kuzidi vyote Afrika Mashariki na kati cha kuzalisha tani 200,000 Mts kwa mwaka na kuajiri watu zaidi ya laki moja (100000) kinajengwa kwenye kata ya mkulazi tarafa ya Ngerengere Jimbo la Morogoro kusini Mashariki Jimbo linaloongozwa na Mhe Mgumba ambaye pia Naibu waziri wa kilimo.
Kiwanda hiki kinaendelea kuleta manufaa makubwa kwa wanachi wa Mkulazi, ngerengere Jimbo la Morogoro kusini Mashariki , Morogoro vijijini Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa ujumla.
Mradi huo unaendelea kuinarisha huduma za jamii kama vile barabara zilizoanza kutengenezwa kutoka Kwaba kwenda Usungura na Barabara ya ngerengere Kidunda itakayoanza kujengwa muda sio mrefu baada ya kupatikana fedha zilizotolewa na Mhe Raisi na serikali ya Dr Magufuli na serikali yake katika kurahisisha shughuli za maendeleo na uendelezaji wa shamba la miwa la mkulazi kwa lengo la kuinua uchumi wa watu eneo hilo pamoja na kumaliza tatizo la upungufu wa sukari nchini.
Katika ziara hiyo Mhe Mgumba aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ndugu Erio, Mwenyekiti wa Bodi ya mkulazi Holding Company Limited Dr Msita, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa uchumi na fedha wa Morogoro Dr Lozaria pamoja na viongizi wa chama na serikali wa wilaya, kata,vijiji na vitongoji wa mkulazi.
Manufaa mengine ya mradi huo ni ajira zilizoanza kupatikana katika kuandaa shamba kwa watu wa Mkulazi, umeme ulioanza kupelekwa kuelekea eneo la mradi, maji , huduma za afya na elimu zinaendelea kuboreshwa kukidhi mahitaji ya wananchi na mradi.
Mhe Mgumba baada ya kumakiza ziara ya Morogoro vijijini ataendelea na kumalizia ziara yake wilayani kilosa leo alhamisi ya Julai 16 mwaka huu.