×

Dayna Nyange Wivu Umeniponza

MWANAMAMA anayefanya poa kunako gemu ya muziki wa Bongo Fleva; Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’ amesema kuwa kinachomfanya aachane na wapenzi wake mara kwa mara ni wivu uliokisiri.

 

Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, mrembo huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Homa, alieleza kwamba akimpata mpenzi, huingia mazima na kujikuta akiathiriwa na wivu.

“Mimi huwa sidumu muda mrefu na wanaume kwa sababu ya wivu, huwa namfuatilia kwa kila kitu, hapo sasa anatakiwa awe makini.

 

“Huwa nahitaji kujua yuko wapi na anafanya nini, nikiona haeleweki naumia na kuona ananiongopea, mwisho wa siku tunaachana,” alisema Dayna Nyange.

Stori:memorise Richard

Leave a Comment