×

Luis: Tutaweka Rekodi Kombe la Shirikisho

KIUNGOmshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone,amefunguka kuwa wataweka rekodi kwenye mechi yao ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA), kwa kucheza kwa juhudi kubwa kama ambavyo walifanya kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Yanga.

Kiungo huyo raia wa Msumbiji ameongeza kuwa watapambana vilivyo katika mechi hiyo kuona wanatwaa ubingwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto zao za msimu huu.

 

Simba watacheza na Namungo FC kwenye mechi ya fainali ya ambayo itapigwa Agosti 2, mwaka huu katika Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

“Kitu kikubwa kwanza tulikuwa na plani katika mechi ya nusu fainali na iliisha kama ambavyo tulipanga iende.“Sasa tuko fainali na tutahakikisha tunafanya makubwa kwenye mechi hiyo kwa sababu tunataka kuchukua ubingwa. Tutapambana kwa nguvu kubwa kuona tunatimiza malengo hayo ambayo tumejiwekea,” alimaliza Luis

Stori: Said Ally,Dar es Salaam

Leave a Comment