×

JPM: Takukuru Msijipendekeze Chato – Video

RAIS John Magufuli ameelezwa kukerwa na kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kuomba fedha kiasi cha shilingi bilioni moja  za kujenga ofisi wilayani Chato mkoani Geita wakati tayari wana ofisi.

 

Magufuli amesema hayo leo, tarehe 22, Julai 2020, wakati akizindua Jengo la Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Chamwino jijini Dodoma ambalo limegharimu kiasi cha Tsh. Milioni 143.

 

“Kwenye taarifa yenu hapa mmesema kuwa mnataka kujenga Ofisi za TAKUKURU Chato mimi nawashangaa, TAKUKURU Chato wana ofisi ya tuliwapa jengo tena la ghorofa lipo juu milimani kwenye shamba la marehemu baba yangu ambalo alinyang’anywa.  Msizungumze mambo kwa kunifurahisha au kujipendekeza, mjipendekeze nikiwa nimeshatoka kwenye urais, this is not the way!

 

“Ninyi watu wa TAKUKURU huku ndiko kung’ata? Mimi natoka Chato na ile ofisi ipo kwenye shamba la marehemu baba yangu alinyang’anywa, ni ghorofa limejengwa na TBA kwa fedha nyingi. Jengo lingine la nini wakati wilaya nyingine hakuna ofisi?

 

“Mnajenga ofisi ya TAKUKURU Chato ya nini? Mlifikiri nitafurahi mkisema Chato? Mimi moyo umeshakuwa sugu. Mkurugenzi hujui kama Chato kuna ofisi ya TAKUKURU? Kwa nini wakudanganye watu wako? Nikiwa Wizara ya Ujenzi, nilimwita Hosea na kukabidhi. Sasa jengo mnaenda kujenga jingine la nini? Haya ni matumizi mabaya ya fedha,” amesema Magufuli.

Leave a Comment