
GARI lililokuwa limebeba Wanachama na Mashabiki wa Klabu ya Soka ya Yanga kutoka tawi la Kidali Asilia, Tandale jijini Dar es Salaam limeopata ajali wakati wakiwa njiani kuelekea Morogoro kushuhudia mechi ya Mtibwa Sugar vs Yanga. Ajali hiyo imetokea Kingorwila nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Uongozi wa Klabu ya Yanga unatoa pole kwa Wanachama na Mashabiki wetu, kutoka tawi la Kidali Asilia Tandale waliopata ajali wakiwa njiani kuelekea Morogoro ambako timu yetu inacheza na Mtibwa Sugar.
Ajali hiyo imetokea eneo la Kingorwila nje kidogo ya mji wa Morogoro imesababisha majeruhi kadhaa na uhalibifu wa mali , hivyo Uongozi unawaombea majeruhi wote wapone haraka.
Uongozi unathamini mchango mkubwa wa Wanachama na Mashabiki katika kuisapoti timu yetu popote inapocheza hapa nchini.
