
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali mohammed Shein, amewasili kwa ajili ya kutoa salamu za pole na kusaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzamia, hayati Benjamin William Mkapa, aliyeaga dunia usiku wa kuamkia jana Julai 24, 2020 jijini Dar es Salaam.
Akimzungumzia Mkapa, Dkt. Shein amesema, “Viongozi waliopo madarakani vijana wanatakiwa wajifunze uongozi wa Mkapa, wajifunze namna alivyoishi na watu, hakubagua watu hata siku moja, wale viongozi wa leo tujifunze kwa marehemu Mkapa
“Mkapa amesaidia sana kuibadilisha nchi, amefanya mabadiliko ya kiuchumi, ameanzisha suala zima la utawala bora, si nchi nyingi za Afrika zina utawala bora, yeye kaanzisha wizara ya mwanzo ya utawala bora hapa Afrika, amesimamia kwa vitendo siyo kwa maneno,” amesemaDkt. Shein.