
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa jana (Ijumaa Julai 24, 2020) alimjulia hali kijana Deogratias Mianga mkazi wa Singida ambaye amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Majaliwa alimwona Deogratias kupitia vyombo vya habari akiomba msaada wa matibabu kutokana na matatizo ya mgongo ambapo Julai 2, 2020, alimfanyia mipango iliyoweza kufikishwa MOI na kufanyiwa upasuaji Julai 6, 2020.