×

Breaking News: Yanga Yamtimua Kocha Wake

KLABU ya Yanga leo, Jumatatu, Julai 27, 2020, imetangaza kumfuta kazi kocha wao, Luc Eymael,  baada ya kocha huyo kusikika akitoa kauli za kibaguzi na zisizo za kimichezo kupitia mitandao ya kijamii na kusambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.

 

Yanga imesema kwamba inafanya kila linalowezekana kocha huyo aondoke nchini mara moja. Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji anadaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi hapo jana.

 

Uongozi wa Yanga umeomba radhi kwa mashabiki wa Yanga viongozi wa shirikisho la mpira nchini Tanzania pamoja na wadau wote wa soka. Yanga imemaliza ligi ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya alama 72.

Kauli alizozitoa Kocha wa Yanga, Luc Eymael Jana Jumamosi na kupelekea kufukuzwa kazi; “Sifurahii nchi hii [Tanzania]. Nyinyi ni watu ambao hamjaelimika. Nimechukizwa. Sina gari, WiFi au DSTV. Mashabiki hawajui chochote kuhusu Soka. Ni kama nyani au mbwa wanavyopiga kelele.”

Leave a Comment