×

Wasifu: Prof. Kabudi Awataja Watoto Alioacha Mkapa – Video

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi, akisoma wasifu wa hayati rais mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa,  amesema  enzi za uhai wake, Mkapa alimuoa Anna na kubahatika kupata watoto wawili wa kiume, Stephano na Nicholas.

 

“Katika ndoa yake na Mama Anna, Hayati Benjamin William Mkapa alijaliwa kupata watoto wawili wa kiume Nicholaus (Nico) na Stephano (Steve) na wajukuu,”  alisema Kabudi katika maelezo yake mafupi ambayo ni pamoja na historia fupi yake ya kikazi.

 

“Hayati Benjamin Mkapa alianza kazi Serikalini kama Afisa Tawala wa Wilaya ya Dodoma Aprili 1962, baada ya miezi minne alijiunga na masomo ya shahada ya uzamili nchini Marekani na aliporudi alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje.

 

“Hayati Benjamin Mkapa alikuwa Rais wa Kwanza kuchaguliwa chini ya mfumo wa vyama vingi ulioanzishwa 1992. Mkapa alifariki kwa ugonjwa wa moyo kusimama ghafla ulioandamana na malaria tarehe 23 Julai 2020 majira ya 3:30 usiku akiwa na umri wa miaka 81.

 

Kabla ya wasifu huo kusomwa na Prof. Kabudi,  Waziri Mkuu alitoa hotuba fupi kwa mujibu wa tukio hilo ambapo pamoja na kuwapa pole Watanzania alimpa pole Rais John Magufuli kwa tukio hilo ambalo limeleta majonzi kwa taifa.

 

“Mheshimiwa Rais niendelee kukupa pole wewe, tukio hili halivumiliki na ni jambo la huzuni ni tukio ambalo hatuwezi kulisahau, kwa sababu mpendwa wetu amefanya kazi kubwa sana nchini na haya yamethibitishwa na Watanzania.”

Leave a Comment