×

JPM Aubadili Uwanja wa Taifa Kuwa Mkapa Stadium – Video

RAIS  John Magufuli amesema kutokana na maombi ya Watanzania  wengi, ametangaza rasmi kuubadili jina Uwanja wa Taifa na kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni sehemu ya kumuenzi rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu ukiwa umejengwa akiwa madarakani.

 

“Hata kwenye michezo alitoa mchango, tena nasikia alikuwa mshabiki mkubwa wa Yanga, ingawa sikuwahi kumsikia akisema hilo hadharani.  Mzee Jakaya Mrisho Kikwete hapa anasema ni kweli kwa sababu na yeye ni Yanga, sifahamu Mzee Mwinyi yeye ni timu gani,” amesema Magufuli na kuongeza:

 

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo, kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’.   Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwa kuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium.”

 

Leave a Comment