×

Aliyepanga Njama za Kumng’oa Rais Mugabe Afariki

WAZIRI wa kilimo wa Zimbabwe Perrance Shiri, amefariki Dunia asubuhi ya jana Jumatano, Julai 29, 2020, wakati akiwa hospitali akipatiwa matibabu, Rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa amethibitisha.

 

“Shiri alikuwa mzalendo wa kweli, aliyejitolea maisha yake kwa ukombozi, uhuru na huduma ya nchi yake,” ameongea Rais wa Zimbabwe Mnangagwa katika taarifa yake japo hakusema chanzo cha kifo.

 

Shiri alikuwa Jenerali mstaafu ambaye alisaidia kupanga njama ya kufukuzwa kwa Robert Mugabe katika mapinduzi ya 2017.

Leave a Comment