×

JPM Apewa Jogoo: ‘Nitakupa Mama Yangu Uwe Baba’ – Video

MWANANCHI mmoja wa Kijiji cha Somanga, wilayani Kilwa, mkoani Lindi, Shaweji Mohamed Kimbwembwe, ameonyesha kufurahishwa na kazi kubwa anayoifanya Rais John Magufuli na kumzawadia jogoo huku akimuomba  rais ampelekee mama yake mzazi kama shukrani kwa kumzaa, kumtunza na kumlea.

 

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi, Julai 30, 2020, wakati Magufuli akizungumza na wananchi hao alipokuwa njiani akirejea jijini Dar es Salaam akitokea Lupaso, Masasi, mkoani Mtwara kwenye mazishi ya rais mstaafu wa awamu ya tatu, hayati benjamin Mkapa ambaye alizikwa jana.

“Mheshimiwa Rais unafanya kazi nzuri sana, kama utaniruhusu nina kuku wangu pale nyumbani nitakuzawadia, mpelekee mama kuku huyu kutoka kwa wananchi wa Somanga, mwambie asante kwa malezi aliyokupa, una moyo mzuri, ni mnyenyekevu, mwadilifu, mchapa kazi, uko vizuri Mheshimiwa Rais, piga kazi,” alisema mwananchi huyo.

Akimpokea jogoo huyo, Magufuli amesema, “Mzee nipe kabisa jogoo wangu uliyenizawadia niondoke naye, nitampelekea mama yangu kama ulivyosema, unajua baba yangu alishatangulia mbele za haki, umetoa jogoo, siku ukienda Chato nitakukabidhi mama yangu na wewe uwe baba, kamlete huyo jogoo , asanteni sana watu wa Somanga.” – Rais Magufuli.

🔴#BREAKING: MAGUFULI APEWA ‘JOGOO’ BURE, AKASIRIKA VIBAYA – “WIZARA ya UJENZI WAMENIUDHI’

Leave a Comment