
DONALD TRUMP ametoa wito kuwa uchaguzi wa rais utakaofanyika Novemba mwaka huu uahirishwe akidai kuongezeka kwa upigaji kura kwa njia ya posta kunaweza kusababisha udanganyifu na matokeo yasiyo sahihi.
Kuna ushahidi mdogo wa madai ya Bwana Trump lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akipinga upigaji kura kwa njia ya posta ambao anadai unaweza kusababisha udanganyifu. Majimbo ya Marekani yanataka upigaji kura kwa njia ya posta kufanywa kuwa rahisi zaidi kwa sababu ya wasiwasi wa matatizo ya kiafya kutokana na janga la corona.
Trump alisema nini?
Katika ujumbe wake kwa njia ya Tweeter, Trump amesema kupiga kura kwa njia ya posta kutafanya uchaguzi wa Novemba kuwa usio sahihi na wenye udanganyifu mkubwa katika historia ya nchi hiyo na aibu kuleta kubwa kwa Marekani.
Alisema hivyo bila kutoa ushahidi wowote kwamba kupiga kura kwa njia ya posta kama inavyofahamika Marekani, kutahatarisha uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni.
“Wanazungumza kuhusu uchaguzi kuingiliwa na nchi za kigeni lakini wanajua kwamba upigaji kura kwa njia ya posta ni njia rahisi ya nchi za kigeni kuuingilia,” amesema.
Alisema njia hiyo tayari inadhihirisha kwamba hilo litakuwa lenye matatizo tu katika maeneo ambayo imejaribiwa. Mapema mwezi huu, majimbo sita ya Marekani yalikuwa yanapanga kufanya uchaguzi wa Novemba kwa njia ya posta: California, Utah, Hawaii, Colorado, Oregon na Washington.
Majimbo hayo yatatuma kura moja kwa moja kwa njia ya posta kwa wapiga kura wote waliosajiliwa, na baada ya hapo zitarejeshwa tena au kuwasilishwa siku ya kupiga kura – ingawa kupiga kura moja kwa moja bado kutakuwepo kwa wachache ambao hali italazimu kufanya hivyo.
Chini ya uchaguzi wa urais, Trump hana mamlaka yoyote ya kuahirisha uchaguzi yeye binafsi na tukio kama hilo ni lazima liidhinishwe na bunge.
Juni, New York iliruhusu raia kupiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa awali wa chama cha Democratic kumtafuta mgombea wa kupeperusha bendera ya chama. Lakini kuhesabiwa kwa kura kulicheleweshwa na hadi kufikia sasa matokeo bado hayajulikani.
Vyombo vya habari vya eneo vimesema kwamba pia kuna wasiwasi kuwa wapiga kura wengi hawatahesabiwa kwa sababu hawakujazwa vizuri au pengine hawana alama zinazoonyesha kwamba kura zao zilitumwa kabla ya siku ya upigaji kura kufikia ukomo wake rasmi. Hata hivyo, kuna majimbo mengi ambayo kwa muda mrefu sasa yamekuwa yakipiga kura kwa njia ya posta.
