
ASKARI waliokuwa wamelewa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamemimina risasi na kuua watu 12 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Mmoja wa wahanga anaripotiwa kuwa mtoto wa miaka miwili. Mauaji hayo yalitokea Alhamisi katika jimbo la Kivu kusini-mashariki mwa nchi hiyo.
Kumekuwa na waandamanaji wenye hasira dhidi jeshi la Kongo katika mji wa Sange, eneo ambalo barabara nyingi zilikuwa zimefungwa.