
WAZIRI wa Afya wa Afrika Kusini, Zwelini Mkhize, amesema maambukizi ya COVID-19 nchini humo yamefikia watu 503,290 baada ya visa vipya 10,107 kurekodiwa juzi.
Afrika Kusini ni nchi ya tano kurekodi idadi kubwa ya maambukizi duniani nyuma ya Urusi, India, Brazil na Marekani. Ni nchi iliyoathirika zaidi na janga la Corona-Virus barani Afrika.
Virusi vya Corona vimesababisha vifo 8,153 nchini humo na wagonjwa waliopona wamefikia 342,461. Mamlaka za afya zimetahadharisha kuwa, maambukizi yanaongezeka kwa kasi.
Wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) lilionya huenda kinachoendelea Afrika Kusini ni taswira ya hali inayoweza kutokea kwa bara zima la Afrika.