×

Hatimaye Mrisho Aanza Kuvaa Viatu “Nimeitwa Mchawi”

MSANII wa tungo za mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto maarufu kama “Mjomba“, ameposti picha mtandaoni ikimuonesha amevaa viatu huku akiwauliza mashabiki zake iwapo aendelee kuvaa viatu au abaki kutembea peku kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote.

 

Mjomba, katika picha hiyo ambayo amepost kwenye ukurasa wake wa Instagram amedai kwamba ameshaitwa mchawi, mshirikina kwa sababu ya imani yake ya kutembea peku bila viatu.

 

“Nimeitwa mchawi, mshrikina na masharti ya mganga kwa kutembea peku, hapo je nirudi peku au nibaki huku,” ameandika Mrisho Mpoto.

 

Ikumbukwe tu msanii huyo alijizolea umaarufu kutokana na style ya kutembea peku popote pale utakapomuona iwe mtaani, studio, mikutano hata akiwa stejini akifanya show na shughuli zingine za kimuziki.

Leave a Comment