STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amelia na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Dk Harrison Mwakyembe katika kusimamia Sera ya Filamu.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Ray amemlilia waziri huyo husika katika tasnia ya sanaa, kwani kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakipambania sera hiyo iwe kwenye katiba ya nchi, lakini suala hilo bado halijatimia.
“Siku zote nimekuwa nikililia kuwepo kwa Sera ya Filamu maana ndiyo ulinzi mkubwa wa kazi zetu.
“Pia kwa muda mrefu sasa wasanii tumekuwa tukipambania sera hii iwe ndani ya Katiba ya nchi, lakini bado haijawa hivyo, namuomba sana waziri wetu Mwakyembe aweke mkazo kwenye suala hili kwa sababu hata wawekezaji huwa wanaangalia sana hilo katika kuwekeza kwenye filamu zetu,’’ alisema Ray ambaye ni nguli wa filamu hapa Bongo.
STORI: HAPPYNESS MASUNGA, DAR
