×

Makonda: Walibweka Kama Mbwa Mwitu, JPM Akaziba Masikio – Video

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Jumatatu, Agosti 3, 2020, amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa huo mpya, Aboubakar Kunenge,  ambapo amemshukuru Rais  John Magufuli kwa kumwamini na kumvumilia.

 

Akikabidhi ofisi hizo, Makonda amesema:

 

Kazi ya uteuzi siyo rahisi ina taarifa na maelezo mengi, lakini Rais Magufuli aliamini katika vijana, nikiwa kijana wa kwanza kupewa majukumu katika mkoa mkubwa na kuacha alama itakayodumu milele yote, namshukuru Rais Magufuli kwa mambo mengi ikiwemo uvumilivu wake.

 

“Ukiteuliwa unaanza kufanya kazi, kazi unayofanya inaweza kuleta kelele na mbwa mwitu wengi wakawa wanabweka lakini Rais wetu aliziba masikio akaendela kuniamini na tarehe 15 nimeondoka mwenyewe ikiwa ni ishara ya kukubali kazi niliyofanya na kuamini ya kwamba sasa umefika wakati uende kwenye majukumu mengine.” amesema Makonda.

 

Aidha  aliongeza kwamba, kazi ya kumtetea rais aliyokuwa akiifanya akiwa mkuu wa mkoa, hataacha kuifanya akitoa onyo kali kwa yeyote atakayemchezea rais.

 

“Msimchezee Dkt Magufuli mkahisi Makonda hatamtetea kwa kuwa hayuko kwenye kiti cha ukuu wa mkoa. Kwa hiyo Mheshimiwa RC, Mambosasa na timu yenu mkihitaji uzoefu wangu katika mapambano ya kumlinda Dkt John Pombe Magufuli, hata kama ni saa tisa usiku nitaamka. Kwangu yeye ni zaidi ya cheo, ni baba,” amsema.

 

Leave a Comment