
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa “Joe Biden anakwenda kinyume na Mungu”.
Trump ameyasema hayo kufuatia kauli ya Biden wa chama cha Democratic akiwa katika majibizano na ‘mtifuano’ uliopo sasa kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo.
Matamshi ya Trump aliyoyatoa wakati wa ziara yake Ohio, yanawadia wakati akijaribu kuingia katika eneo muhimu la majimbo ya Midwestern ambako kulikuwa na mchango mkubwa katika kupata ushindi wake 2016.
Biden, mwenye imani kubwa ya Kikatoliki, atakuwa anakabiliana na Trump katika uchaguzi wa Novemba. Kura za maoni zinaashiria kwamba hivi sasa chama cha Democratic kiko mbele.
Trump ameshutumiwa kwa kutumia mtindo wa siasa za kurusha maneno katika mjadala uliofadhiliwa na fedha za walipa ushuru unaolenga kuzungumzia sera za serikali ya Marekani.