
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas leo Agosti 7, 2020, ame pato la taifa limekua kwa kasi kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi, sera nzuri za fedha na matumizi stahiki
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Dkt. Abbas amesema kwamba takwimu za miaka minne zinaonyesha kwamba pato la taifa limekua kwa wastani wa TZS Trilioni 124.0 kwa mwaka ikilinganishwa na wastani wa TZS Trilioni 52.9 kwa mwaka katika miaka 10 ya Awamu ya Nne (2006-2015).
Pato la Mtanzania mmoja mmoja limeongezeka sana kutoka wastani wa Dola za Marekani 622.0 (TZS 979,513) mwaka 2015 hadi Dola 1,063.3 mwaka 2019/20 (TZS 2,386,000) – Dkt.Hassan Abbasi

Katika miaka mitano ya Rais Magufuli, Pato la Taifa limekua kwa kasi kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi, sera nzuri za fedha na matumizi stahiki
Katika miaka minne (2016-2019) uchumi wetu umekua kwa wastani wa asilimia 6.9 kwa mwaka, wastani ambao ni wa juu ikilinganishwa na awamu zote

Mapato ya Serikali yameongezeka kutoka wastani wa TZS Bilioni 850 kwa mwaka 2015, TZS Trilioni 1.3 mwaka 2016 hadi 2018/19 na Julai 2019, hadi Juni 2020 tumefikia wastani mpya wa TZS Trilioni 1.5 (ambapo Desemba 2019 na Juni 2020 tumekusanya TZS Trilioni 1.9)
Mapato yasiyo ya kodi nayo yameongezeka kutoka TZS Bilioni 688.7 mwaka 2014/2015 hadi kufikia TZS Trilioni 2.4 mwaka 2018/2019. Haya ni matokeo ya kubana mianya ya kukwepa kodi.

Katika miaka minne na miezi 10, Serikali ya Awamu ya Tano imeweka rekodi ya kupunguza mfumuko wa bei kutoka wastani wa 9.2% mwaka 2015 hadi 4.3% mwaka 2019/20
Kila Mtanzania ashiriki katika maendeleo ya uchumi kwa kufanya kazi kwa bidii, kulipa kodi, kushiriki kutumia fursa zinazojitokeza, kutoa maoni stahiki kwa Serikali na vyombo vyake katika kuboresha uchumi wetu

Tunapaswa kufuata misingi ya kimaadili wakati huu ili kuzidi kuimarisha uchumi kama ifuatavyo, tuepuke rushwa, uvivu kazini, tuache tabia za “kisebusebu na kiroho papo” yani mtu kuwa wamoto-baridi kwa wakati mmoja
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx