×

Sakata la Morrison TFF Yasema Nyaraka Hazijatimia – Video

MWENYEKITI wa Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji, Elias Mwanjala, amesema leo wameshindwa kufikia maamuzi ya sakata la mkataba kati ya Bernard Morrison na Yanga kutokana baadhi ya nyaraka muhimu kutoka pande zote mbili  kushindwa kupatikana, hivyo wataendelea tena kesho, Agosti 12, 2020.

 

Wanjala amesema kuna nyaraka moja ambayo Yanga SC hawajaiwasilisha na nyaraka nyingine ambayo Morrison hajaiwasilisha, hivyo zitawasilishwa leo jioni na watakaa tena kesho asubuhi na kutoa maamuzi.

 

“Wahusika wametuhakikishia document hizo tutazipata leo jioni, kwa hiyo kesho saa 2:30 tutaanza kikao,  mpaka saa 7 tutakuwa tumefikia maamuzi. Mpaka sasa ni hamsini kwa hamsini, nadhani nimeeleweka.  Maneno ya mtaani achaneni nayo, ukweli tunao sisi, muwe na subira kila kitu tutawaeleza,” amesema Wanjala.

 

Leave a Comment