×

Mavoko Afunguka Kusainiwa na Harmonize – Video

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko, ameweka bayana kuhusu stori zilizosambaa kwamba anataka  kusainiwa na msanii mwenzake aliyekuwa naye WCB, Harmonize katika lebo yake ya Kondegang.

 

Mavoko ameeleza kuwa yeye ameshangazwa na hizo habari mtandaoni na kuongeza kuwa huenda Harmonize alijisikia tu kuandika kwa sababu ni mtu ambaye tangu zamani alikuwa rafiki yake hata wakati yupo WCB.

 

Mbali na hilo  amezungumzia kuhusu kutumia akaunti yake ya Rich Mavoko ambayo iliaminika ipo chini ya WCB na kuhusu kutumia nyimbo alizofanya chini ya Diamond Platnumz.

 

Leave a Comment