
HATMA ya kocha mkuu mpya wa Yanga katika msimu ujao inatarajiwa kujulikana leo mara baada ya mabosi wa timu hiyo kukutana kupitia majina ya makocha waliotuma maombi ya kumrithi Mbelgiji, Luc Eymael.
Jumla ya makocha 64 hadi hivi sasa ndio waliotuma CV wakiomba kibarua cha kukinoa kikosi hicho kwenye msimu ujao, kati ya hao ni Mrundi, Ettiene Ndayiragije, Mholanzi Hans Pluijm na Mbrazili, Marcio Maximo.
Yanga hivi karibuni ilimfukuza kazi Mbelgiji huyo baada ya kutoa lugha ya ubaguzi kwa mashabiki wa timu hiyo. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi huo unatarajiwa kukutana leo jioni kwa ajili ya kupitia CV hizo za makocha kabla ya kufanya mchujo na kumpata mmoja kutokana na sifa wanazozitaka.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumpata kocha huyo mwenye vigezo na sifa wanazozitaka, haraka watamtangaza Jumatatu ya wiki ijayo siku ambayo timu hiyo itaingia kambini kwa ajili ya kuanza pre season.
“Hatma ya kocha mkuu na msaidizi inatarajiwa kujulikana kesho (leo) baada ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Yanga kukutana na kupitia maombi na CV.
“Baada ya kupitia ma-jina yote haraka wataufanya mchujo na kumpata kocha mmoja atakayekuwa kocha wetu katika msimu ujao am-baye tutamtangaza Jumatatu ya wiki ijayo,” alisema mtoa taarifa huyo.
Mkurugenzi Uweke-zaji wa GSM, Injinia Hersi Said alithibitisha hilo juzi kwa kusema kuwa: “Wiki ijayo tutam tambulisha kocha wetu mara baada ya kupitiamao mbi yao waliyoyatuma kwe nye klabu na tumepokea mao mbi ya makocha kutoka Afrika na Ulaya.”
STORI: WILBERT MOLANDI, DAR ES SALAAM