×

Mlipuko wa Beirut: Mawaziri 3, Wabunge 9 Wajiuzulu

WAZIRI wa Habari, Manal Abdel Samad na Waziri wa Mazingira, Damianos Kattar, wamejiuzulu kufuatia mlipuko wa Agosti 04, 2020,  uliosababisha vifo 157 na majeruhi 6,000.

 

Kufuatia mlipuko huo uliotokea eneo la bandari ya mji wa Beirut, maelfu ya wananchi waliandamana mwishoni mwa wiki iliyopita kushinikiza viongozi kujiuzulu.

 

Katika taarifa yake, Manal amesema anajiuzulu kwa heshima ya waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na ambao hawajulikani walipo. Pia, ameongeza kuwa amefanya hivyo kuitikia wito wa wananchi kutaka mabadiliko.

 

Mbali na mawaziri hao, wabunge wapatao tisa nchini humo wamejiuzulu tangu kutokea kwa mlipuko huo ambao umepelekea watu wapatao 300,000 kukosa makazi. Wataalamu wanakadiria kuwa mlipuko huo umesababisha hasara ya takriban Dola Bilioni 15.

Leave a Comment