BENKI Kuu imetoa dokezo la kisera (fedha) kudhibiti zaidi upatikanaji wa fedha za kigeni. Sera hii inapunguza upatikanaji wa fedha za kigeni kwa ajili ya miamala ya kimataifa (export revenue) na kitaifa au kuharamisha biashara za fedha za kigeni kupitia mitandao kwa miezi sita ijayo.
Katika sera hii mpya viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vitaanzia Dola 250,000 mpaka 50,000 (Takriban Tsh. zaidi ya Milioni 580 mpaka 100) kwa miezi sita ijayo.
Pia, mabadilishano ya fedha kati ya benki na benki hayatakiwi kuzidi kiwango cha Dola 250,000 (saidi ya Tsh. milioni 580) katika muamala mmoja. Sheria hizi ambazo zimeanza kufanya kazi Agosti 7, 2020, pia zinazuia benki kufanya miamala yoyote na wateja ambao hawana akaunti katika benki husika.


