×

Mgombea UMD Aahidi Maisha Laini si Kama Ugali Uliolala

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa UMD, Khalfan Mohamed Mazurui na Mgombea Mwenza, Mashavu Alawi Haji katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 10, 2020. Chama hicho kinakuwa cha kumi na mbili (12) kuchukua fomu.

 

Mazururi anasema lengo la chama chake ni kuwaletea wananchi wake maendeleo, maisha laini, na siyo maisha magumu kama ugali ambao umelala.

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25, 2020.

Leave a Comment