The House of Favourite Newspapers

Rasmi Yanga Yamsajili Farid Kwa Miaka Miwili

0

Yanga SC imetangaza rasmi leo Agosti 12, 2020 kukamilisha usajili wa winga wa Kimataifa wa Tanzania, Faridi Mussa Shaha kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru kutoka Club Deportivo Tenerife ya Hispania.

Usajili huo wa Mussa sasa unamfanya kuwa nyota wa nane kusajiliwa na Yanga msimu huu akitanguliwa na kiungo Zawadi Mauya (Kagera Sugar), mabeki Bakari Mwamnyeto (Coastal Union), Yassin Mustapha (Polisi Tanzania).

Wengine ni mabeki Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar), Abdallah Shaibu (Ninja), washambuliaji Waziri Junior (Mbao) na Yacouba Sogne (Asante Kotoko) huku kiungo Feisal Salum naye akiongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Leave A Reply