×

Chama Afichua Jambo Simba

CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji anayekipiga ndani ya Simba, amefichua kwamba kilichombeba zaidi kwa msimu wa 2019/20 ni juhudi zake binafsi pamoja na kumtegemea Mungu.Msimu wa 2019/20, Chama alichaguliwa kuwa mchezaji bora na kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo alihusika kwenye mabao 12 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba.

 

Chama alifunga mabao mawili katika Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City na Alliance, huku akitoa asisti 10.

“Kwangu mimi mpira ni kazi yangu, ni kitu ambacho ninakipenda ndio maana ninafanya yote ndani ya uwanja. Ninawaheshimu watu wote na ninafikiria kwamba watu wote ni bora kwa namna wanavyofanya.

 

“Heshima pia ni kitu cha msingi bila kusahau kwamba ninamwamini Mungu jambo ambalo linanifanya ninakuwa bora pamoja na kupata ushirikiano kutoka kwa wenzangu.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, DAR ES SALAAM

Leave a Comment