MWIMBAJI nguli wa nyimbo za taarab, Mzee Yusuf ameibukia katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuungana na wasanii wenzake pamoja na wakeleketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuzindua nyimbo maalum zitakazotumika katika Kampeni za chama hicho kwa mwaka huu.
Mzee Yusuf amepafomu nyimbo zake huku akiamsha shangwe kwa mashabiki ikiwa ni siku chache tangu amerudi rasmi kwenye game ya muziki baada ya kukaa nje ya game kwa miaka kadhaa akimtumikia Mungu.
