×

Video: Adam Mchomvu Amlima Mtama Mbasha “Ananiita Bangi?”

MTANGAZAJI wa Clouds Media, Adam Mchomvu ‘Baba Jonii’ ameshindwa kujizuia na kujikuta akimshusha stejini kwa bonge la mtama, mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha katika Tamasha la Uhuru Kuna Jambo ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamezindua nyimbo zitakazotumika katika kampeni zao za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

 

Akizungumza na Global TV Online baada ya tukio hilo, Adam Mchomvu amesema amekereka na kitendo cha Mbasha kumita Adam kuwa yeye ni ‘Bangi’.

 

“Nilikuwa sijui kama huyu jamaa ni mduwanzi kiasi hiki, kumbe ndiyo maana aliachwa na mke wake, nipo pale stejini nina host shoo ananiita mimi Bangi tena si mara moja. Kumbuka hii shoo inatazamwa LIVE na watu wengi kuanzia Mhe. Rais mpaka watu wa kawaida.

 

“Nimetengeneza jina langu kwa muda mrefu anakuja kuniharibia brand yangu ndani ya dakika chache, bado sijamalizana naye, nitamtafuta private halafu nitajua kitakachoendelea,” amesema Mchomvu.

 

Aidha, kwa upande wake, Mbasha amezungumza baada ya kupigwa mtama na Mchomvu ambapo amesema haoni kosa alilomfanyia Mchomvu mpaka ampige mbele za Watu na amejisikia vibaya sana lakini amemsamehee na amemuachia Mungu.

TAZAMA VIDEO HAPA

Leave a Comment