
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao leo Agosti 16, 2020 ametambulisha jezi rasmi za Azam FC za msimu ujao.
Jezi nyeupe itakuwa ya nyumbani, bluu itakuwa ya ugenini huku ya orange ikiwa ya ziada (neutral).
Kidao mbali na kutambulisha jezi pia ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa wiki ya Chamazi iliyoanza rasmi leo, ambayo itaitimika Jumapili ijayo kwa Tamasha la Azam Festival.
