×

Ronaldo Ajiandaa Kutimka Old Trafford Dirisha Dogo la Usajili, Ten Hag Abariki

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo

NYOTA wa soka wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza Cristiano Ronaldo anajiandaa kutimka klabuni hapo majira ya usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari mwaka huu.

 

Taarifa zinadai kuwa nyota huyo anachukua maamuzi hayo akiwa na lengo la kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwani msimu huu amekuwa akiishia benchi kwenye michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa hivi karibuni wa Manchester Dabi ambao klabu yake iliambulia kichapo cha mabao 6-3.

Erik Ten Hag, Kocha wa Manchester United

Kwa mujibu wa Jason Burt Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Telegraph la nchini Uingereza ameripoti kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Mholanzi Erik Ten Hag amesema hawezi kumzuia nyota huyo kutimka klabuni hapo endapo tu klabu itapokea ofa nzuri.

 

Tayari CR7 ameshaweka wazi nia yake ya kuendelea kucheza soka kwa muda mrefu akiwa na malengo ya kushiriki mashindano ya Fainali za Euro zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2024.

Leave a Comment