×

Breaking: Yanga Yamalizana na Kisinda wa AS Vita

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Klabu ya Yanga imemalizana na AS Vita na kumsajili nyota wa wao raia wa Congo DR, Tuisila Kisinda ambaye ni mshambuliaji.

 

Shughuli hiyo imefanyika jijini Kinshasa, DRC na Yanga imewakilishwa na Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa uwekezaji wa Kampuni ya GSM.

 

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu kumekuwepo na tetesi za mara kwa mara kwamba Yanga wanamsajili kinda huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye inasemekana alikuwa ni pendekezo la aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Luc Aymael.

Leave a Comment