The House of Favourite Newspapers

Kauli ya Masele Baada ya Kupigwa Chini Ubunge

0

Jana, Alhamisi, Agosti 20, 2020 Kikao Cha Halmashauri Kuu Kuu ya CCM Taifa (NEC) kimetangaza Majina ya Wagombea Ubunge kwenye Majimbo watakaopeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2020.

 

Muda mfupi baada ya majina kutangazwa,Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele (2010-2020) ambaye aliongoza katika uchaguzi wa kura maoni CCM kwa kura 152 amesema amepokea kwa heshima maamuzi ya chama chake kumtangaza Patrobas Katambi aliyeshika nafasi ya 7 kwa kura 12 katika kura za maoni kuwa mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu 2020.

 

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter,Stephen Masele ameandika ujumbe ufuatao:

 

“Nimepokea kwa heshima kubwa maamuzi ya chama changu. Nawashukuru wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini, viongozi wote wa chama changu ngazi zote kwa kunipa fursa ya kuwa mbunge kwa miaka kumi. Tushikamane kukipigania chama kiweze kushinda uchaguzi mkuu. Binafsi nitashiriki kikamilifu,” – Stephen Masele.

 

Leave A Reply