“TUTAWAFUNGA mpaka mchakae.” Hiyo ni moja ya kauli ya mashabiki wa Yanga wanajinasibu nayo baada ya timu yao kufanya usajili wa maana hasa kwenye safu ya ushambuliaji.
Yanga katika safu ya ushambuliaji, kwa usajili iliofanya, imekusanya mabao 50 kutoka kwa mastaa wao wapya wa safu hiyo.
Katika usajili wao huo, Yanga imejiimarisha kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo safu ya ushambuliaji ambapo tayari imewavuta kikosini hapo Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo ‘Carlinhos’ kutoka Angola, Yacouba Songne (Burkina Faso), Michael Sarpong (Ghana) na straika mzawa, Wazir Junior.
Washambuliaji hao wanne katika timu walizotoka, wamemaliza msimu wa 2019/20 katika ligi zao wakiwa na jumla ya mabao 50 jambo ambalo linaipa faida Yanga kuanza msimu ikiwa na washambuliaji wenye uchu mkubwa wa mabao.
Sarpong aliyetoka Rayon Sport ya Rwanda, msimu uliopita alifunga mabao 16, Waziri Junior aliyekuwa Mbao FC, alifunga mabao 13.
Yacouba Sogne aliyekuwa Asante Kotoko ya Ghana, alifunga mabao 12, huku Carlinhos katika kikosi cha Petro de Luanda pale nchini Angola, akifunga mabao tisa na kutoa asisti tano.
Carlinhos mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa kufunga, pia ni mpishi mzuri wa mabao Nyota wote tayari wameungana na wenzao kambini katika maandalizi ya msimu ujao kasoro Carlinhos na Sogne ambao muda wowote kuanzia sasa wanaweza kutua hapa nchini na kuanza kazi rasmi ndani ya kikosi hicho.
Jana Jumamosi katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar, Sarpong alifi ka kwa mara ya kwanza akiwa na nyota wengine wa kimataifa kutoka DR Congo, winga Tuisila Kisinda na kiungo mkabaji, Mukoko Tonombe.Wachezaji hao walifi ka kwa ajili ya kuungana na wenzao kuanza kazi rasmi
ya kuifanya Yanga kurudisha nguvu yao ya kutwaa mataji kama zamani. Mbali na wachezaji hao, pia aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha Mazingisa ambaye kwa sasa ni muajiriwa wa Yanga, naye alifi ka mazoezini hapo kwa mara ya kwanza.
Sarpong alisema: “Kitu cha kwanza ninafurahia kuwa hapa baada ya kujiunga na wenzangu. Nimeona mashabiki ambavyo wamenipokea na nawaahidi tutafanya kitu kizuri kwa ajili yao.”Wakati huohuo, taarifa kutoka Yanga zinasema kuwa,
Kocha Cedric Kaze raia wa Burundi, mapema wiki ijayo atatua hapa nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo akichukua mikoba ya Mbelgiji, Luc Eymael.
Yanga kwa sasa inafanya mazoezi chini ya kocha wa viungo, Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini ambapo program hizo za mazoezi anazipokea kutoka kwa Cedric Kaze



