Shoo Ya Jide ilivyofunika Mlimani City Alfajili Ya Leo
Mkongwe wa Bongo Fleva, Lady Jaydeee Komando, usiku wa kumkia leo alipiga bonge la shoo kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar akisherehekea kutimiza miaka 20 kwenye gemu.
Shoo hiyo ilihudhuriwa na nyomi la mashabiki ambapo mwanamuziki huyo aliwanogesha ile mbaya.
Shoo hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Bongo muvi, Bongo Fleva na wengine ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Geofrey Mungereza a.k.a Mzee wa Rungu la Maadili naye alikuwepo akiifutilia kiumakini shoo hiyo.
Baadhi ya mastaa walihudhuria ni wasanii wa Bongo muvi, Kajala Masanja, Steve Nyerere, Mwanamitindo Flaviana Matata na wengine wengi.
Jide akikamua na AY.
HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPLÂ Â