×

Shonza Awataka Tunduma Kumchagua Silinde

Mteuliwa wa Ubunge viti maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, amewataka wananchi wa Tunduma kumchagua mgombea wa CCM, David Silinde ili afungue milango ya maendeleo katika ukanda huo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Shonza ametoa kauli hiyo jana Septemba 6, wakati akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa kampeni wa Silinde katika mji wa Tunduma mkoani Songwe.


Aidha, Shonza aliwashambulia makada wa Chadema wanaodaiwa kuhusika na mauaji wa MwanaCCM Brighton Mollel kwa kuongezea kuwa laana ya mauaji ya kijana huyo ni Wanatunduma kuwanyima kura wagombea wote wa Chadema sambamba na mgombea wao Frank Mwakajoka.

“Silinde ni Mbunge msomi mwenye nidhamu na mchambuzi wa mambo na mpenda maendeleo sio Mwakajoka ambaye hawezi hata kuongea bungeni na hana elimu ya kuongoza eneo muhimu kama hilo la Tunduma,” alisema Shonza.

NA MWANDISHI WETU, TUNDUMA

Leave a Comment