×

Umati Ulivyofurika Uzinduzi wa Kampeni Za Fella Kilungule, Wasanii Kibao

Wasanii wa nyimbo za asili wakitumbuiza.

Meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platniumz’ jana alisababisha mafuriko makubwa ya watu wakati akizindua kampeni zake za kutetea kiti chake cha Udiwani wa Kata ya Kilungule, Mbagala Jijini Dar.

Muimba taarab, Athuman Soud a.k.a Prince Amigo akikamua kabla ya Mkubwa Fella kupanda jukwaani.

Katika uzinduzi huo Mkubwa Fella alimwaga sera zake huku akieleza mambo mengi aliyoyafanya kipindi chake kilichopita ikiwemo kuongeza madarasa kwenye shule za msingi na sekondari pamoja na ujenzi wa shule ya Msingi Martin Lumbanga ulipofanyika uzinduzi huo.

Kiongozi wa Kundi la Vuvuzela Modern Taarab, Aisha Othman akikamua kwenye uzinduzi huo.

Mengine ni uchimbaji wa visima na kumaliza shida ya maji kwenye kata hiyo, ujenzi wa barabara za mitaa na mengineyo.

Mkubwa Fella akiomba kura kwa Wanakilungule.

Pamoja na utamu za sera hizo, uzinduzi huo ulinogeshwa na wasanii mbalimbali wa bongo fleva, taarab na ngoma za asili.

Umati ukimsikiliza Mkubwa Fella.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment