
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Simon Msanjila, leo amelipongeza Shirika la Madini la Taifa ‘STAMICO’ kwa utendaji wake bora wa hivi karibuni na kufikia kuipa serikali gawio la shilingi bilioni 1.1.

Profesa Msanjila amelipongeza shirika hilo alipokuwa mgeni rasmi wakati akifungua mkutano wa 6 wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo.

Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtengaji wa Shirika hilo, Dkt. Venance Mwase alimuelezea jinsi shirika hilo lilivyopambana na changamoto mbalimbali ikiwemo malipo ya likizo kwa wafanyakazi na mengineyo ambayo kwasasa tatizo hilo halipo tena.
Dkt. Mwase amesema miongoni mwa mafanikio ya shirika hilo kupata tenda ya kuchoronga dhahabu ambayo anadhani itazidi kuinua kipato katika shirika hilo.

Kufuatia kumaliza changamoto katika shirika hilo na kufikia mafanikio hayo mgeni rasmi mpongeza Mkurugenzi huyo na wafanyakazi wake kwa mafanikio hayo kufikia kuipatia serikali gawio hilo la bilioni 1.1
Profesa amewasisitiza wafanyakazi hao kuzidi kuchapakazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa na si kuangalia mafanikio yao binafsi.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL