×

Nafasi ya Kazi Mhandisi wa Baharini, Ministry of Works, Transport and Communications

POST MHANDISI WA BAHARINI (MARINE ENGINEER) – 1 POST
POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION
EMPLOYER Ministry of Works, Transport and Communications
APPLICATION TIMELINE: 2020-09-09 2020-09-23
JOB SUMMARY NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.    Kufuatilia, kutathmini na kushauri kuhusu utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ufanisi;
ii.    Kutoa ushauri wa kisera na kisheria kuhusu teknolojia bora ya ujenzi na uendeshaji wa Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na TEMESA;
iii.    Kusimamia tafiti zinazohusu usanifu, ujenzi na matumizi ya Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na TEMESA;
iv.    Kutoa ushauri wakitaalam kuhusu namna ya kudhibiti uharibifu wa Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na TEMESA;
v.    Kufuatilia na kushauri kuhusu utekelezaji wa Mikataba na Maazimio mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ya uendeshaji salama wa Vivuko vya Serikali;
vi.    Kufanya ukaguzi na kuandaa taarifa ya haliya Vivuko vya Serikali na kushauri ipasavyo;
vii.    Kukusanya na kuchambua taarifa za utekelezaji wa miradi ya Vivuko na mapato yanayotokana na uendeshaji wa Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na  TEMESA;
viii.    Kufanya uainishaji wa kiufundi (technical specification) wa viwango (standards) vya ujenzi wa Vivuko vya Serikali vinavyosimamiwa na  TEMESA;na
ix.    Kufanya utafiti na kushauri kuhusu maegesho ya Vivuko vya Serikali kwa ajili ya matumizi ya Umma.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi wa Baharini (MARINE ENGINEERING).
REMUNERATION TGS E

 > CLICK HERE TO APPLY <

Leave a Comment