×

Maxrioba: Mimi Si Meneja Tena wa Wema, Mobeto

ALIYEWAHI kuwa meneja wa Hamisa Mobetto, Max Rioba, ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye si meneja wa Hamisa Mobetto tena wala wa Wema Sepetu ila anafanya nao kazi tu.

 

Max amedokeza kuwa katika tamthilia yake ya WE MEN wameanza mazungumzo na wasanii wa nje kama P Square kutoka Nigeria Casper Nyovest kutoka Afrika Kusini na Saut Soul kutoka Kenya ili waanze kufanya nao kazi kwenye tamthilia hiyo.

 

Lakini pia Max akiwa mtu wa karibu wa Wema Sepetu ametoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kati ya wasanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Batuli, kujibizana mitandaoni hadi kusababisha Batuli kumpost Wema na kuandika maneno ambayo yalionekana kutomfurahisha.  Max ametoa maoni yake na kusema kinachotakiwa ni heshima na Batuli hakupaswa kuandika maneno kama yale kwa msanii mwenzake.

Leave a Comment