The House of Favourite Newspapers

Shirikisho la Muziki lampongeza Rais Magufuli

0

addo

Rais Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo November Mwasongwe.

Ndugu wanahabari leo hii tarehe 12 Novemba 2015 nimekuiteni hapa Kwenye ofisi zetu hapa Mlimani City kwa ajili ya mambo machache.

Nisingependa kuwapotezea Muda wenu mwingi Maana Sasa tunaongozwa na kauli Mbiu ya Hapa Kazi Tu hivyo ni bora tukae Muda mfupi na kwenda kuchapa Kazi Tu.

Ndugu wanahabari nimekuiteni kutoa pongezi za dhati na kuunga mkono kasi aliyoanza nayo ndugu Magufuli siyo tu ameonesha kutosha Kwenye Kiti bali amekuwa mtetezi wa wanyonge.

Ndugu wanahabari Ziara za Ghafla za Ndugu Magufuli siyo za kubezwa Ni za kupongezwa sana. Japo kuna wenye roho mbaya na wasioitakia mema nchi yetu wanabeza maana wao walizoea kubweteka na kufurahia wanyonge wakiteseka.

Shirikisho la Muziki Tanzania tumeona matunda ya Rais Magufuli juzi amekwenda Muhimbili na Jana tangazo limetoka kuwa mashine za MRI zimeanza Kufanya Kazi hili jambo si la kubezwa hata kidogo bila jitihada binafsi za Ndugu Magufuli leo watanzania wangeendelea kufa na kukata tamaa kwa kukosa matibabu.

Ndugu wanahabari haikuwa rahisi kwa wakati Kama huu ambao Ni wa Kupanga serikali mpya bado Rais ametoa Muda wa kwenda kuhakikisha wanyonge wanapata matibabu na huduma tuna pongezi sana Ndugu Magufuli.

Wembe Ni ule ule aendelee na Ziara hizo za kushtukiza maeneo mengi yana uozo azibe mianya ya wakwepa kodi hasa Kwenye madini ambako tuna Mikatana mibovu iliyoingiwa na wasio na Huruma, wizi na usafirishaji haramu wa madini, Ni Jambo la aibu Tanzanite kwa wingi ipo Kenya na Afrika Kusini na kodi hatukupata ipasavyo na kwingine kwingi Kama Kwenye mbuga za wanyama na utalii ambapo wanyama wanauwawa kwa Faida ya wachache Jambo hili ni la kulivalia njuga na mengine mengi.. Kwa kuziba mianya hiyo na kuleta maendeleo ya wote hakika hatutahitaji misaada ya wazungu.. Tupo tayari kufunga Mkanda kwa miaka hii mitano ili kuacha hazina kwa Taifa letu lenye kila aina ya utajiri.

Jambo la kumalizia tunamtakia afya tele na tunaahidi ushirikiano kwake Kwenye haki za wanamuziki Kama alivyotuahidi pale Mlimani City vile vile Tunamuombea kwa Mungu apate Baraza la Mawaziri dogo lenye ufanisi na kupunguza mzigo kwa serikali Kama dhamira yake alivyoionesha Kwenye kuondoa safari za Nje vile vile Tunamuombea kwa Mungu asiogope vitisho vya Chura Yeye anywe Maji. Maji Ni kuwaletea maendeleo watanzania.

Hali hii ya kasi ya Magufuli itawafanya Diasporas wote wakumbuke kuwekeza nyumbani maana Sasa wanajua hazina zao zitakua salama maana mwadilifu anaongoza nchi. Naomba nichukue nafasi hii kuwatoa hofu watanzania waishio ughaibuni kuwa nchi ipo Salama na Dereva wetu kwa Sasa ni Makini kweli kweli.

Zaidi ya yote ninapongeza wasanii wote walioshiriki Kwenye kampeni za vyama mbali mbali Sasa kampeni zimeisha Ni Muda wa Kufanya Kazi tuwe wamoja.. Rais wetu Ni Magufuli tuvunje Makundi kwani siasa siyo uadui Ni Muda wa kujiletea maendeleo yetu wenyewe!

Ndugu wanahabari Sasa Tunaandaa Mkutano Mkubwa wa Amani na Maandamano ya kuunga Mkono Hatua za Magufuli kwa kweli tuna Imani naye na tunaamini Mungu atamuwezesha kuyatimiza yote na kukata Kiu ya watanzania.

Nakutakieni Kazi njema,
Wenu
Addo November Mwasongwe
Rais Shirikisho la Muziki Tanzania

Leave A Reply